Full-Width Version (true/false)


Mtoto kutoka Kenya aliyemkuna Alicia Keys kwa kuimba wimbo wake wa ‘Girl On Fire’ aachia video ya wimbo wake wa kwanza
Mwezi uliopita kwenye tasnia ya burudani nchini Kenya kuliibuka mtoto ambaye video zake zilisambaa mitandaoni zikimuonesha akiimba wimbo wa ‘Girl On Fire’ wa Alicia Keys kwa kiwango cha hali ya juu. Sasa mtoto huyo tayari ameachia video yake ya wimbo wake wa kwanza.

Mtoto huyo ajulikanaye kwa jina la Gracious Amani ameachia wimbo huo unaoitwa ‘Sitasahau’ ambapo ameelezea safari yake fupi ya muziki huku akiwashukuru watu wote walimsaidia hadi kutoka hapa alipo kwa sasa.

Video ya wimbo huo imeongozwa na Director Young Wallace na mdundo wa ngoma hii umetengenezwa na Teddy B. Tazama video mpya

No comments

Powered by Blogger.