Full-Width Version (true/false)


Mtu mmoja ameuawa na wananchi wenye hasira kali katika jaribio la wizi wa Ngombe.
Habari:Mtu mmoja ameuawa na wananchi wenye hasira kali katika mtaa wa Amani kata ya Nkuhungu jijini Dodoma akiwa katika jaribio la kutaka kuiba ngombe ,huku watu wengine watano wakikimbilia kusikojulikana mara baada ya kutekeleza jaribio hilo ambapo Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma linaendelea kuwaska wahalifu hao na kuwataka wananchi kutii sheria bila shuruti. 

mwandishi wetu amefika eneo la tukio na kukuta baadhi ya wananchi wakishuhudia mwili wa mtu huyo pamoja na kidhibiti alichokutwa nacho ambapo mtu huyo inadaiwa alijaribu kuiba ngombe huyo majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo ambapo baadhi ya mashuhuda wamesema matukio ya wizi wa mifugo katika eneo hilo yamekuwa yakishika kasi hivyo wameamua kujichukulia sheria mkononi. 

Kwa upande wake Mmiliki wa  ngombe amesema si mara ya kwanza watu kijitokeza na kuiba mifugo katika eneo lake ambapo amesema watu hao huwa wanatumia mbinu mbalimbali za wizi ikiwemo kupuliza sumu ya usingizi na kuiomba serikali kuimarisha ulinzi ili kupunguza vitendo vya uhalifu. 

Akizungumza kuhusu tukio Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa polisi Gilles Muroto amesema jeshi hilo linaendelea na misako mbalimbali ya kuwatafuta wahalifu huku akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watii sheria bila shuruti.

No comments

Powered by Blogger.