Full-Width Version (true/false)


Mume amuacha mkewe aliyedumu nae miaka 14, kisa Lionel Messi

Moja kati ya stori za kusisimua katika soka barani Ulaya ni pamoja na hii stori ya mwanaume wa kirusi kuachana na mke wake wa ndoa aliyedumu nae kwa miaka 14 kutokana na mkewe kukosoa uwezo wa Lionel Messi wakati wa fainali za Kombe la Dunia.

Arsen mwenye umri wa miaka 40 na Lyudmila mwenye umri wa miaka 37 wameachana kufuatia mke wake kuwa shabiki mkubwa wa Cristiano Ronaldo na kupenda kumkosoa Lionel Messi ambaye anashabikiwa na mmewe Arsen.


“Kwa mara nyingine tena alipoanza kuzungumza maneno yake yasiofaa kuhusu Lionel Messi na kukosoa uwezo wake nikapata hasira na kumgeukia na akaendelea kueleza kila kitu ambacho kinasifia u-handsome wa Ronaldo”>>> Arsene


Arsen na Lyudmila kwa mara ya kwanza walikutana 2002 katika bar nchini Urusi wakifuatilia Kombe la Dunia na miaka miwili baadae walifunga ndoa, wote wawili ni mashabiki wa Club ya Moscow lakini nje ya hapo mumewe ni shabiki wa Barcelona na mkewe shabiki wa Real Madrid na Cristiano Ronaldo, wawili hao wameachana wiki iliyopita baada ya ugomvi wao mkubwa mkewe kukosoa uwezo wa Messi wakati wa Kombe la Dunia.

No comments

Powered by Blogger.