Full-Width Version (true/false)


Muuza nyama ya paka apunguziwa hukumu

 

MAHAKAMA ya Nakuru imepunguza hukumu inayomkabili mtu ambaye alipatikana na hatiua ya kuuza nyama ya paka.

Hakimu Joel Ngugi alipunguza hukumu ya jela miaka mitatu hadi miaka miwili , akieleza kwamba James Mukangu Kimani atatumikia adhabu ya jela kwa awamu ya mwaka mmoja na baadae miwili kutokana na kukabiliwa na mashtaka mawili hadi sasa.

Aidha hukumu hiyo pia ilibainisha kuwa Hakimu Mkuu Bernard Mararo alikosea kwa kumtoza Kimani faini ya shilingi 50,000 badala ya shilingi 10,000 kwa kosa la pili.

Kimani alishitakiwa kwa kuchinja na kuuza nayama ya paka kwa wateja ambao hawakujua kwa mtumizi ya binadamu kinyume cha sharia mnamo Juni 24 katika mji wa Nakuru.

Aidha anakabiliwa na shitaka la kuchinja wanyama katika eneo ambalo halina viwango vinavyotakiwa.

Alikamatwa wakati akimchuna ngozi paka na kuwaleza wanahabari kuwa aliuza zaidi ya paka 1,000 kwa wauza sambusa na mahoteli mbalimbali jijini tangu mwaka 2012.

Alisema aliamua kufanyabiashara hiyo baada ya kugundua kuwepo kwa pengo la biashara hiyo sokoni.

Hata hivyo, wateja wake ahawakubaini kwamba alikuwa akiwauzia nyama ya paka. DAILY NATION

No comments

Powered by Blogger.