Full-Width Version (true/false)


Mwanamke aliyepiga picha na mume wa Muna aibukaSIKU chache baada ya kusambaa picha ‘romantic’ za mume wa muigizaji wa filamu Bongo, Rose Alphonce ‘Muna’, Peter Zacharia akiwa na mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la Rehema katika mitandao ya kijamii, mwanamke huyo ameibuka na kufungukia picha hizo huku akiwashangaa wanaozivalia njuga.

Akifanya mahojiano na Ijumaa Wikienda, Rehema alisema kwamba anamjua aliyezisambaza picha hizo ila kiufupi Muna atambue yule baba ni mtu mzima na yeye aliondoka kwa hiyo asingeweza kuvumilia kuishi bila ya kuwa na uhusiano.


“Jamani Peter ni mtu mzima siyo mtoto, Muna atambue kuwa aliondoka kwake hivyo asingeweza kuishi mwenyewe,” alisema Rehema.


Kumekuwa na maneno mengi mitandaoni kuhusu picha zinazosambaa mitandaoni zikimuonyesha Peter na Rehema katika mapozi ya kimahaba siku chache baada ya kumzika mtoto wake, Patrick.

No comments

Powered by Blogger.