Full-Width Version (true/false)


Mwarabu Fighter afunguka ishu ya kufukuzwa WCB


Baunsa anayemlinda Msanii wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ anayefahamika zaidi kwa jina la Mwarabu Fighter amefungukia tetesi zinazosambaa mitandaoni zikidai kuwa amefukuzwa kazi na nafasi yake imeshikiliwa na mtu ambaye tunamuona hivi sasa akiwa anamlinda Mbongo fleva huyo.

Mwarabu amekanusha tetesi hizo na kusema kuwa bado yupo WCB na anaendelea kufanya kazi na Diamond kama kawaida, kutokumuona naye ni kwa sababu ya taratibu za kiofisi ambazo hawezi kuziweka wazi ila siku yoyote tutamuona naye.

Mwarabu amefunguka hayo alipokuwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokwenda kutoa nyuzi alizowekewa siku chache zilizopita baada ya kupata ajali.

No comments

Powered by Blogger.