Full-Width Version (true/false)


Mwigulu Nchemba amnadi Tlaghasi, uchaguzi wa madiwani Babati
Babati. Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Singida, Mwigulu Nchemba amemnadi mgombea udiwani wa kata ya Bagara Nicodemus Tlaghasi (CCM).
Nchemba ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, amemnadi Tlaghasi jana Julai 18 akiwa na mbunge wa jimbo la Babati Vijijini Vrajilal Jituson.
Wawili hao walitinga viwanja vya mtaa wa mji mpya kata ya Bagara na kumnadi mgombea huyo.
Akizungumza wakati wa kumnadi mgombea udiwani huyo Mwigulu amewaomba wakazi wa eneo hilo kumchagua ili kumuunga mkono Rais John Magufuli kufanikisha maendeleo nchini.
"Maendeleo yote yanayofanyika nchini ni utekelezaji wa ilani ya CCM hivyo msipotoshwe na wapinzani hapa Babati wanaojinadi kuwa watatekeleza maendeleo hizi barabara za lami na miradi ya maji ni kazi ya Rais Magufuli," amesema.
Tlaghasi alijiuzulu nafasi hiyo hivi karibuni akiwa diwani wa kata hiyo  kupitia  Chadema akidai kuwa anaunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa huo Alexander Mnyeti.

No comments

Powered by Blogger.