Full-Width Version (true/false)


Mwili wa Yassoda kuagwa Dar leo
MWILI wa aliyekuwa Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Juliana Matagi Yasoda utaagwa leo Jumapili tayari kusafirishwa kwenda kuzikwa kesho Jumatatu wilayani Mpwapwa, mkoani Dodoma.
Yassoda alifariki dunia Alhamisi iliyopita muda mfupi baada ya kuwasili ofisini kwake Wizara ya Elimu, jijini Dar es Salaam alikokuwa amehamishiwa akiwa Ofisa wa Idara ya Shule za Sekondari.
Dada wa marehemu, Georgina Richard alisema zoezi la kuaga mwili wa Yasoda litaanza saa 5:00 asubuhi nyumbani kwa marehemu Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
“Baada ya zoezi hilo saa 9 alasiri safari ya kwenda Mpwapwa itaanza kwa ajili ya kumpumzisha kwenye nyumba ya milele ndugu yetu siku ya Jumatatu,” alisema.
Yasoda alikutwa na mauti baada ya kuanguka akiwa kwenye ghorofa ya kwanza ya ofisi za wizara hiyo akipandisha ngazi kwenda ofisini kwake.
Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Maimuna alisema alifika ofisini akiwa mzima akiwa anaendesha gari mwenyewe.

No comments

Powered by Blogger.