Full-Width Version (true/false)


Mzee Mwinyi atoa neno kwenye maonesho ya Sabasaba


Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amesema soko bora la bidhaa huanzia katika nchi husika kwa wakazi wa nchi hiyo kuipenda bidhaa ama huduma husika na kisha bidhaa ama huduma hizo kusambazwa nchi nyingine.


Alhaji Mwinyi amesema hayo katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Julius Nyerere wakati akifungua siku ya mwani na viungo katika maonesho hayo ya biashara ya Kimataifa na kuongeza kuwa kutokana na hilo ni lazima watanzania wapende bidhaa zinazolishwa hapa nchini.


Naye Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Balozi Amina Salum Ally amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka mkazo katika zao la mwani na viungo kutokana na kutambua umuhimu wake katika ukuaji wa pato la taifa.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Biashara ya nje – TANTRADE Edwin Rutegeruka amesema mamlaka hiyo iliamua kutenga kila siku kuwa siku ya kitu fulani ili wadau wa kitu hicho waweze kupata fursa ya kujadiliana kwa kina.

No comments

Powered by Blogger.