Nape Asema Hana Mpango wa Kuhama CCM.....Mtazame Hapa Alivyojumuika na Wapiga Kura Wake Kutazama Kombe la Dunia
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema hawezi kukihama chama hicho tawala kwa kuwa ana hisa nyingi.
Nape ametoa kauli hiyo jana jioni Jumapili Julai 15, 2018 mbele ya wananchi wa Mtama ambao jioni hiyo alijumuika nao kutazama fainali za kombe la Dunia..
Amewataka
wananchi hao kuondoa hofu juu yake akiwataka kupuuza maneno yanayosemwa
kuhusu hatima yake CCM ambapo alisisitiza kuwa hataondoka katika chama
hicho.
Kuhusu
asilimia 65 ya ushuru wa zao la korosho kwenda Serikali Kuu, Nape
amesema ataendelea kufuatilia jambo hilo na kusisitiza kuwa kuteleza si
kuanguka.
No comments