Full-Width Version (true/false)


Nauli za ndege mpya Boeing 787-8 Dreamliner hizi hapa, sawa na bure

 

Kufuatia ujio wa ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner ambayo inatarajiwa kuanza safari zake wiki tatu zijazo tayari nauli za kupanda ndege hiyo zimeweka bayana ambapo gharama zimetajwa kuanzia Shilingi 93,000 tu kwa safari moja.
Hata hivyo ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 262 inatarajia kuanza safari zake Julai 29, 2018 kuanzia Dar es salaam kuelekea Kilimanjaro na kisha kuelekea Mwanza na kutoka Mwanza ndege hiyo itakuwa inaruka kuelekea Kilimanjaro na kurudi jijini Dar es salaam kila siku kwa mwezi mzima.
Hizi ndio gharama za nauli ya ndege mpya Boeing 787-8 Dreamliner.
Dar – Mwanza  shilingi 113,000 pamoja na kodi kwa sufari moja,  lakini kwenda na kurudi ni shilingi 206,000.
Kilimanjaro – Mwanza  shilingi 93,000 kwa safari moja, kwenda na kurudi ni shilingi 166,000.
Dar es salaam – Kilimanjaro  shilingi 98,000 kwa safari moja, kwenda na kurudi  ni shilingi 176,000.
Aidha ndege hiyo inatarajiwa kurushwa na marubani 8, ilitua jijini Dar es salaam Jumapili iliyopita na kupokelewa na watanzania wakiongzwa na Rais John Pombe Magufuli.

No comments

Powered by Blogger.