Full-Width Version (true/false)


Ngassa atamba kuipaisha Yanga

 

 
Baada ya kurejea Yanga akitokea Ndanda FC ya Mtwara, Mrisho Ngassa anaamini atairejesha katika makali yake kama ilivyokuwa zamani.
 


Winga huyo aliyewahi kutamba miaka ya nyuma akiwa na kikosi hicho chini ya Nahodha, Nadir Haroub, Cannavaro, amesema bado ana uwezo wa kucheza hivyo atajitahidi kuonesha kile ambacho anacho.
 

"Nina uzoefu na mashindano ya Ligi Kuu, sidhani kama nitashindwa kuonesha uwezo wangu, nitalionesha hilo Uwanjani" alisema Ngassa.
 

Ngassa tayari ameshaanza kujinoa na kikosi cha Yanga ambacho kimeweka kambi katika Uwanja wa Chuo cha Polisi uliopo Kurasini jijini Dar es Salaam.
 

Ikumbukwe kikosi hicho kipo kwenye maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika na Julai 18 kitacheza dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

No comments

Powered by Blogger.