Full-Width Version (true/false)


Ngassa rasmi arejea Yanga na kukabidhiwa uzi wake...
Kiungo mkongwe nchini Mrisho Ngassa amerejea Yanga rasmi na kukabishiwa jezi mbele ya wanahabari.

Ngassa amerejea na kujiunga na Yanga tena baada ya safari yake ndefu ndani na nje ya nchi.
Kiungo huyo mtoto wa kiungo wa zamani wa Simba, Khalfan Ngassa, aliondoka Yanga na kwenda Afrika Kusini alipojiunga na klabu ya Free State Stars, lakini hakudumu aliporejea nchini na kujiunga na Mbeya City.

Baada ya Mbeya City alihamia Ndanda FC baada ya mpango wake wa kurejea Yanga kushindikana lakini kwa ajili ya msimu ujao, inaonekana mambo ni safi kwake.

No comments

Powered by Blogger.