Full-Width Version (true/false)


Nilimwambia Jux ole wako uvae ‘kikuku’ – Vanessa Mdee
Je wewe unaweza mruhusu mpenzi wako wa kiume avae kikuku?. Muimbaji Vanessa Mdee amemchimba biti mpenzi wake Jux kuingia kwenye anga hizo.Vee amedai uvaaji wa vikuku sio utamaduni wa wanaume wa Kitanzania hivyo hawezi pendezwa na utamaduni huo kwa madai umamshushia heshima mwanaume.

“Kusema kweli Jux hawezi kuvaa kikuku ,” Vanessa aliiambia Wasafi TV. “Sidhani kama inaendana na tamaduni zetu. Vikuku ni kwaajili ya wasichana, sipendi japo naona kuna watu wengi wanavaa,”

Aliongeza, “Kiukweli kuna msanii wa Marekani anampenda Jux anaitwa Fabulous, na yeye nahisi anavaa kikuku, nikasema nini hiki, nikamwambia ole wako na wewe uvae.,”

Wawili hao kwa sasa wanafanya vizuri na tour yao ya muziki iitwao ‘In Love and Money’.

Katika hatua nyingine, mapema leo muimbaji Diamond Platnumz amepokea madongo kutoka kwa mashabiki wake mtandaoni baada ya kuonekana amevaa kitu ambacho kinaonekana kama ni kikuku.

No comments

Powered by Blogger.