Full-Width Version (true/false)


Nimekoma kuwa kiongozi kwenye misiba: Steve Nyerere

MSANII maaru­fu wa vichekesho Bongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema amekoma kuwa kiongozi misibani kwa sababu ya matusi anayovuna akishika nafasi hiyo.
 

Steve aliiambia  Za Motomoto News  wikiendi iliyopita kuwa, amekuwa akijitoa kwenye misiba ya wasanii wenzake lakini licha ya wema wake huo amekuwa akivuna skendo za ajabuajabu (kama ulaji fedha za rambirambi) na matusi jambo ambalo linamhuzunisha na kuiathiri familia yake.
 

“Unajua mimi nina wa­toto, sasa wanapoona ya­nayoandikwa mitandaoni ya kunitukana na kunifedhehesha kwa vitu vya uongo wa­tanichukuliaje, niseme tu huu msiba wa mtoto Patrick Peter ambaye ni mtoto wa msanii mwenzangu Muna ndiyo wa mwisho, sitajihusisha tena na uongozi; kwenye misiba nita­shiriki kama mtu wa kawaida,” alisema Steve.

No comments

Powered by Blogger.