Full-Width Version (true/false)


Nusu Fainali Ya Kwanza Ya Kombe la Dunia 2018 ni Leo Kati ya Ufaransa na Ubelgiji

Nusu ya fainali ya kwanza ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi inaanza leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika Uwanja wa Saint Petersburg baina ya Ufaransa na Ubelgiji.

Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na asilimia kubwa ya wadau wengi soka duniani itaanza majira ya saa 3 kamili usiku wa leo.

Mpaka sasa Ufaransa waliowahi kutinga hatua ya fainali mwaka 2006 dhidi ya Italia, wamepewa asilimia kubwa ya ushindi kuliko wapinzani wao Ubelgiji.

Ufaransa na Ubelgiji zimekutana mara 73 katika mashindano yote huku Ubelgiji wakishinda mara 30 na Ufaransa wakishinda mara 24 pamoja na kwenda sare mechi 19, leo watakuwa wanakutana mara ya 74.

Vilevile timu hizi kukutana mara ya mwisho katika michuano hii ilikuwa ni mwaka 1986 ambapo Ufaransa iliweza kushinda mabao 4-2 katika hatua ya kusaka mshindi wa tatu.

Na katika mchezo wa mwisho ambao ulikuwa wa kirafiki, Ubelgiji waliibuka na ushindi wa mabao 4-3 jijini Paris, mwaka 2015.

Kesho kutakuwa na mchezo mwingine wa pili ambapo England iliyokuwa haipewi nafasi kubwa kufanya vizuri, itakuwa inacheza na Croatia.

No comments

Powered by Blogger.