Full-Width Version (true/false)


Pamoja na mkwara wa Simba, meneja wa Fei Toto asisitiza kuwa Simba walimfuata kiungo huyo
Pamoja na Simba kuweka msisitizo haitaki kuhusishwa na suala la kiungo Feisal Salum maarufu kama Fei Toto, meneja wake, amesisitiza, Simba walimfuata.


Meneja Mohamed Kombo ambaye pia ni Meneja wa JKU, amesema anajua Simba walimfuata Fei Toto.

Kombo maarufu kwajina la Afande Chomody amethibitisha mchezaji wake kufuatwa na Simba na Singida United kwa ajili ya kufanya naye mazungumzo.


Kiungo huyo alitamburishwa baada ya kuingia mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea Yanga katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki.

“Kuanzia leo (jana) Fei Toto ni mchezaji halali wa Yanga ni baada ya Yanga kufuata kanuni za usajili wa mchezaji wangu kwa kuanza kufanya mazungumzo na wamiliki wa mchezaji mwenyewe ambao ni JKU.


“Zipo baadhi ya timu zilimfuata kwa ajili ya mazungumzo ikiwemo ikiwemo Simba na Singida United ambayo yenyewe tunasakia ilimsajili bila ya sisi kujua chochote kama wamiliki wa mchezaji huyo,”alisema Afande Chimody.


Leo, Msemaji wa Simba, Haji Manara amesisitiza kwamba watachukua hatua kama atatokea mtu kuwahusisha na suala la Fei Toto.

Manara “ametupa” mkwara akisisitiza kwamba Simba haihusiki na suala hilo na isingependa kuona inahusishwa.

No comments

Powered by Blogger.