Full-Width Version (true/false)


Panga la maana lapita Lipuli

UNAWEZA ukashangaa wachezaji wanapata mahitaji yao japokuwa si kwa ukamilifu fulani, lakini linapokuja suala la uwanjani, mambo ni tofauti kabisa. Sasa sikia hii, klabu ya ya Lipuli FC imewatema wachezaji 15 iliokuwa nao msimu uliopita wa Ligi Kuu.
Taarifa ya klabu hiyo ilisema kuwa wachezaji hao wamepigwa chini kwa kushindwa kuonyesha kiwango cha kuridhisha kwenye ligi hiyo msimu uliopita.
Miongoni mwa nyota waliopewa mkono wa kwaheri ni makipa Agathon Mkwambo na Fadhili Butamu na sasa wamebaki na kipa mmoja Mohamed Yusuph.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Lipuli FC kupitia kwa Ofisa Habari wao, Clement Sanga ni kwamba kamati ya usajili kwa sasa inasaka magolikipa wawili kwa ajili ya kuziba pengo hilo ambapo kocha mkuu Seleman Matola amependekeza kikosi chake kiwe na jumla ya wachezaji 25.
‘‘Msimu uliopita tulikuwa na wachezaji 28 ambao baada ya kuwatema hao tumebakiwa na wachezaji 13 hivyo kwa usajili huu wa wachezaji wapya tuna mahitaji madogo kwa ajili ya kufunga milango ya usajili,’’.
Sanga alisema wapo katika hatua nzuri ya mazungumzo na wachezaji wanaowahitaji lakini kutokana na vurugu zilizopo kwenye klabu juu ya usajili wanahofia kuwataja kwa majina kwa kuogopa kuporwa.
“Kuna wachezaji tunao, tunaamini watatusaidia, lakini kwa mazingira yaliyopo, hatutaki kuwataja kwa kuwa wapo wababe wa usajili na wanaweza kutupora, kwa hiyo usajili utabakia na utaratibu wa klabu.
‘’Kocha alikuwa hapa Iringa kwa muda wa wiki tatu zilizopita kwa ajili ya kusaini mkataba mpya pia kukabidhi ripoti kwa viongozi juu ya wachezaji wapya , lakini kuanzia Jumatatu (kesho)anaweza kurejea kuendelea na majukumu yake kwa kuwa tunataka kuanza maandalizi mapema,” alisema Sanga.

No comments

Powered by Blogger.