Full-Width Version (true/false)


Pluijm ndiye pekee aliyesajili Bara

 

NYOTA wa zamani wa Yanga na Mchambuzi wa soka nchini, Ally Mayay ametazama kikosi cha Azam FC kilivyo na kutamka, Kocha Hans Pluijm ndiye pekee aliyeshirikishwa na kuhusika moja kwa moja kwenye usajili wa timu.
Mayay alisema tofauti na Simba na Yanga, zinazoonekana asilimia kubwa ya usajili wao unafanywa na viongozi tena kwa mihemko ya kuwafurahisha mashabiki, Azam wamefanya usajili kulingana na mahitaji ya timu ndio maana anamfagilia Pluijm.
“Fuatilia wachezaji waliosajiliwa Simba na Yanga ni wale waliokuwa wanatajwa kwenda mojawapo ya timu hizo, kwa hiyo mmoja anapowahiwa anaona mjanja bila kujali mahitaji ya kocha atakayekiongoza kikosi hicho.
“Mfano Simba wanatafuta kocha mkuu na tayari wamefanya usajili, unajiuliza je akija kocha mpya watafanyaje ikitokea kikosi atakachokabidhiwa si hitaji lake, hiyo ndio changamoto ya klabu kongwe, kwani hata Yanga ndicho wanachokifanya.” Alishauri klabu za Ligi Kuu kuwa waangalifu msimu ujao kwa kusajili na kuandaa timu zao wakijua kuna ongezeko la mechi kutoka 30 za msimu uliopita kwani idadi ya timu zimetoka 16 hadi 20 kwa maana kila timu itacheza mechi 30 sasa.

No comments

Powered by Blogger.