Full-Width Version (true/false)


Polisi Morogoro yaonya madereva wanaoleta ujanja ujanja


Kufuatia operasheni za mara kwa mara zinazofanywa na jeshi la polisi  mkoani Morogoro  kwa magari yaendayo mikoani zimeanza kuleta matokeo ambapo jumla ya leseni 4,734  zimekaguliwa na  madereva tisa wamefikishwa mahakamani  kati yao watano  wamehukumiwa kifungio cha miezi minne jela na faini ya shilingi elfu kumi.

Akizungumza  mara baada ya kugagua magari yaendayo mikoani katika kituo cha mabasi  Msamvu Morogoro kamanda wa polisi  mkoani hapa  Wilbrod Mutafungwa  amesema  zoezi hilo la  ukaguzi wa magari ni endelevu     hivyo wamewafikisha mahakamani  Madereva Tisa ambao kati yao  watano wamehukumiwa kifungo cha miezi  minne jela na faini ya shilingi elfu kumi  ili iwe fundisho kwa madereva wengine

Pia kamanda Mutafungwa amewataadharisha abiria  ambao wanatabia ya kumshawishi na kushabikia dereva kuendesha kwa mwendokasi kuacha tabia hiyo kwani zoezi hilo ni muhimu  sana kwa ni linaokoa maisha yao

Kwa upande wa mmoja wa madereva wa mabasi Hashim Mohamedi Jamila Peter wamelishukuru jeshi la  polisi  wameshauri  zoezi hilo liwe enderevu pia litolewe kwa madereva wote  pia suala la muda lilikizingatiwa

No comments

Powered by Blogger.