Full-Width Version (true/false)


Polisi nchini India wapigwa marufuku kuwa na vitambi

Leo July 11,2018 nakusogezea stori kutoka huko nchini India ambapo unaambiwa kuwa Kamanda mmoja wa Jeshi la Polisi nchini humo aitwae Bhaskar Rao amewataka Maafisa wake wa Polisi kupunguza uzito wa miili yao na kuacha kunenepa kupita kiasi la sivyo atawasimamisha kazi.

Imeelezwa kuwa Kamanda huyo amechukua uamuzi huo baada ya Askari wake 100 kufariki ndani ya miezi 18 iliyopita kutokana na kutojali afya zao.

Duru za kuaminika zinasema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la Askari wa nchini humo ambao wamenenepa kupita kiasi kitu kinachohatarisha maisha yao na ufanisi wa kazi yao.

Aidha Kiongozi huyo amesema kuwa Askari hao watapewa msaada ili kuhakikisha wanapunguza uzito wao wa miili yao.

No comments

Powered by Blogger.