Full-Width Version (true/false)


Profesa Ndalichako awataka TCU kuongeza makali kuvibana vyuo vikuu.

 

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh. Prof Joyce Ndalichako ameiagiza Tume ya vyuo vikuu nchini TCU kuongeza kasi ya kuhakiki ubora wa vyuo vya elimu ya juu na vitakavyobainika kukosa vigezo hata kiwe cha serikali kifungiwe kwani suala la ubora wa elimu  ni jambo la lazima kwani  hakuna haja ya kuwa na msururu  wa vyuo visivyokuwa na tija. 

Prof.Ndalichako ameyasema hayo alipokuwa akifungua maonyesho ya vyuo vikuu ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi. 

Wakati akizundua maonyesho hayo Prof Ndalichako amevitaka Vyuo vikuu kutafuta suluhu changamoto zinazoikumba jamii  na  kuonyesha fursa  mbalimbali zilizopo katika sekta ya kilimo,viwanda ambapo baadhia ya vyuo vimemweza kuhusu tati walizofanya katika maeneo hayo. 

Katika maonyesho hayo baadhi wanafunzi wamejitokeza kupata taarifa za namna ya kujiunga na vyuo vya ndani na nje ya nchi na kupatiwa maelezo ya kina.

No comments

Powered by Blogger.