Full-Width Version (true/false)


Raia wa India ambaye hajakata kucha kwa miaka 66

Leo July 11,2018 nakufikishia stori hii kutoka huko nchini India ambapo Raia wa nchi hiyo aitwae Shridhar Chillal hatimaye ameamua kuzikata kucha zake za mkono ambazo alikuwa hajazikata kwa miaka 66.

Chillal alianza kuzifuga kucha hizo toka mwaka 1952 na anashikilia rekodi ya Guiness kwa kuwa Mtu mwenye kucha ndefu zaidi duniani huku kucha zake zikitajwa kuwa na urefu wa sentimita 909.

Aidha kwa sasa Chillal ana miaka 82 na ameona ni muda sahihi wa kuzikata kucha zake hizo ambapo imedaiwa kuwa atafanya tukio hilo kwenye jengo moja la makumbusho nchini humo.


No comments

Powered by Blogger.