Full-Width Version (true/false)


RAY VANNY aachana na ushindani wa mavazi na mastaa wenzake


Msanii wa muziki kutoka lebo ya muziki ya WCB Wasafi, Rayvanny ameiambia Dizzim Online kuwa anaamini ushindani upande wa mavazi anabaki kuwa yeye ni mwenye ujuzi na yuko katika viwango vya kuvaa vitu vya gharama zaidi hivyo hahitaji tena kushindana.

Akizungumzia hatua ya kutotaka tena kujihusisha na ushindani wa mavazi, Rayvanny aliongeza kuwa kwa sasa ana mambo mengi ya maana ya kufanya ikiwemo kujikuza zaidi kimuziki na kuandaa maisha mazuri ya mwanae JayDan kwa sasa na siku za Usoni.

Kwa sasa Rayvanny anafanya vizuri na wimbo wake mpya kwa jina ‘Chombo’, ambapo pia amegusia kuwa kutokana na mapokezi mazuri ya audio ya wimbo huo, mashabiki watengemee kupokea video ya wimbo huo muda wowote kuanzia sasa

No comments

Powered by Blogger.