Full-Width Version (true/false)


RC Mjini Magharibi ampa maagizo mazito RPC

Mkuu wa mkoa wa mjini wa mjini magharib unguja Ayoub Mohammed Mahoud  amemuagiza kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa mjini magharibi kumshikilia kwa mahojiano zaidi kaimu mkuu wa soko la matunda na mboga mboga la Mombasa Hassani Ali Hassani Kutokana na kushindwa kutoa ufafanuzi juu ya malalamiko ya wafanyabiashara katika soko hilo.


Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa wa mjini magharibi Unguja wakati akifanya ziara yake katika soko hilo la mboga mboga na matunda Zanzibar ikiwa na lengo la kusikiliza matatizo yanawakabili wafanyabiashara mbali mbali katika soko hilo


Ayoub alisema hatua hiyo ameichukua mara baada ya kuona majibu na kauli wanazopatiwa kutoka kwa kaimu mkuu wa soko haziridhishi juu ya malalamiko ya kunyanyaswa na kutopatiwa baadhi ya ufumbuzi kwa kero zinazowakabili  wafanyabiashara hao.


 “Hatuwezi kuona watu wachache walipewa dhamana fulani wanawanyanyasa wananchi kutokana na unyonge wao” alisema RC Mahoud.


Aidha Mkuu wa mkoa alisema katika ziara hiyo  amebaini kuwepo kwa unyanyysaji mkubwa kwa wafanya biashara ambapo wafanyabiashara huamishwa katika maeneo yao bila ya kupewa taarifa zilikuwa rasmi kutoka katika uongozi wa soko hilo.


Pia alisema kuwa amebaini kuwepo kwa  udandanyifu mkubwa wa ukusanyaji wa mapato kwa wafanyabiashara kwani kuna muda mrefu wafanya biashara wamekuwa wanalipa kodi katika maeneo yao ya kufanyia biashara na bila kupatiwa risiti hivyo kwa tafsiri ya serikali pesa hizo zimekuwa zikiishia mifukoni mwa watu.


Hata hivyo amewataka wafanya biashara katika soko hilo kuwa wavumlivu na kuafuata sheria zilizowekwa huku serikali ikihakikisha inatatua changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili sokonii hapo.


Kwa upande mwigine ameagiza wafanya biashara hao kujiorodhesha majina kwa wale ambao walivunjiwa maeneo yao kutokana ukarabati wa soko hil ambapo mara baada ya kukamilika kwa ukarabati huo wameshindwa kurudishwa katika maeneo yao ya awali na kutolewa nje ya soko.


Hata hivyo mkuu wa mkoa aliwaagiza wafanya biashara hao kutokuwa oga katika kutoa taarifa ya kero ziazowakabili sokoni hapo ili kuweza kupatiwa ufumbuzi kwa haraka.


Nae mfanyabiashara Said Mohammed Ali alipongeza  hatua hiyo iliochukuliwa na mkuu huyo wa mkoa na kuomba serikali kurakisha kuwatatulia changamoto zinazowakabili haraka ili waendeleee na shughuli zao kama kawaida sokoni hapo.


Katika ziara hiyo ya mkuu wa mkoa wa mjini magharib unguja ikiwa ni muendelezo wa kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi ameagiza jeshi la polise kuhakiksha wanapa ufunguo wa ofisi ya mkuu wa soko ili kufanya ukaguzi na kuweza kujiridhisha zaidi.


No comments

Powered by Blogger.