Full-Width Version (true/false)


Ronaldo hatocheza game ya Juventus vs Real Madrid August 5 2018

Siku ya August 5 2018 Fedex Field Washington club ya Juventus aliyojiunga nayo staa Cristiano Ronaldo itacheza dhidi ya Real Madrid kwa mara ya kwanza baada ya kumnunua Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.

Juventus watacheza game yao ya pili ya International Champions Cup dhidi ya Real Madrid August 5, huku taarifa kutoka Marca zikieleza kuwa staa wao mpya Cristiano Ronaldo hatocheza game hiyo dhidi ya timu yake ya zamani.

Sababu iliyoelezwa kuwa inaweza kumfanya Ronaldo hasicheze mchezo huo ni kutokana na kuwa atakuwa amefanya mazoezi siku chache toka awasili, hivyo asingependa kucheza game yake ya kwanza dhidi ya timu yake ya zamani ya Real Madrid akiwa hayuko fiti kwa aslimia 100.

Ronaldo alimaliza kuitumikia timu yake ya taifa ya Ureno katika michuano ya World Cup 2018 June 29 na anategemea kuwa ataungana na timu yake baada ya mapumziko July 30, Ronaldo atakuwa kafanya mazoezi na wenzake kwa siku 5 kabla ya kucheza dhidi ya Real Madrid ikiaminika kuwa ni siku chache sana.

No comments

Powered by Blogger.