Full-Width Version (true/false)


Rwanda yaitishia TanzaniaTimu ya Taifa ya Wanawake Rwanda yaitishia Kilimanjaro Queens kuelekea mchezo wao wa ufunguzi wa CECAFA wa wanawake ambao umepangwa kupigwa kesho Julai 19, 2018 nchini humo. 

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa timu Wanawake ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Queens',  Bakari Shime amesema mechi hiyo haitakuwa rahisi kwa kuwa wenyeji wao ambao ni Rwanda wamepania kupata ushindi kwenye
mechi hiyo.


"Mchezo wa Rwanda tunategemea utakuwa mchezo mgumu kwasababu Rwanda ni wenyeji na kwa vyovyote vile wamejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba wanalibakisha kombe nyumbani lakini kimsingi ni kwamba pamoja na wao kuwa nyumbani sisi tunaamini tutafanya vizuri zaidi mbele ya mashabiki zao kwa kuwa ni mabingwa", amesema Shime.

Mbali na hilo, Kocha huyo amekataa kuzungumzia mchezo wao unaofuata baada ya Rwanda kwa kuwa akili zao zote wamezielekeza kwenye mchezo wao wa kesho ambao ndio wa kwanza kwenye mashindano hayo ya CECAFA dhidi ya  wenyeji Rwanda.

Msikilize hapa chini Kocha Mkuu wa timu ya Wanawake ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Queens", Bakari Shime akielezea zaidi juu ya mchezo huo.

No comments

Powered by Blogger.