Full-Width Version (true/false)


Said Fella aanika mshahara anaolipwa na DiamondMeneja nguli wa muziki wa kizazi kipya ambaye hivi sasa anasimamia biashara ya muziki wa Diamond Platnumz, Said Fella ameweka wazi kiasi cha mshahara anaolipwa na Bosi huyo wa WCB, kwa asilimia.
Fella ambaye pia ni diwani, amesema kuwa hupokea asilimia 30 ya pato lote lililoingia kutokana na muziki wa Diamond kila mwezi bila kujali mamilioni yatakayokuwa yamepatikana.
“Mshahara wangu ni asilimia 30 ya pato la kila mwezi analoingiza Diamond kwa muziki wake. Haijalishi ameingiza shilingi ngapi, hata kama ni milioni 800,” alisema Fella.
Akizungumzia hatua ya mameneja wa Diamond kuanza kuweka wazi mishahara wanayolipwa, alisema kuwa hii inatokana na kufuata sera ya Rais John Magufuli ya kuwa wazi.
“Mheshimiwa Rais Magufuli sasa hivi amesema ni lazima tuwe wazi. Kama unachosema unacho, kama hauna sema hauna. Usilazimishe kuwa hauna useme unacho au unacho useme hauna. Kwahiyo, naona kuweka wazi inakuwa sawa kwasababu mwisho wa siku hata yule mtu anayedhani kuwa uko pale afahamu kuwa sio hivyo uko hapa,” aliongeza.
Mkubwa Fella ana historia kubwa kwenye muziki wa kizazi kipya, akiwa ndiye meneja wa kwanza wa Juma Nature aliyesaidia mafanikio makubwa ya kimuziki katika safari ya mwimbaji huyo.
Fella anaendelea kushika historia ya kuyapa mafanikio makubwa makundi ya Wanaume Family, Yamoto Band na mengine huku akiwaibua na kuwaweka kwenye kilele cha muziki wasanii tangu wakiwa na umri mdogo kama ilivyokuwa kwa Aslay.

No comments

Powered by Blogger.