Full-Width Version (true/false)


Simba miaka saba makocha kumi
Dar es Salaam.Wakati Simba ikimtangaza kocha mpya Mbelgiji Patrick Aussems leo jijini Dar es Salaam, rekodi zinaonyesha mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wameajili makocha kumi (10) katika kipindi cha miaka saba (7).
Rekodi hiyo ni ya tangu msimu wa 2011/2012 ambapo Simba ilitwaa ubingwa  ikiwa chini ya Mserbia, Milovan Cirkovic na kuusotea kwa miaka mitano mfululizo bila mafanikio hadi msimu huu ilipotwaa ikiwa chini ya Mfaransa, Pierre Lechantre.
Hata hivyo, Simba iliachana na kocha huyo ambaye bosi wa klabu, Salim Abdallah 'Try Again' alisema Lechantre aliondoka baada ya kumaliza mkataba na tayari alikuwa ameomba kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Cameroon hivyo hawakuona sababu ya kuendelea naye.
Mfaransa huyo alikuwa ni kocha wa tisa kuinoa Simba katika kipindi cha miaka saba akichukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog aliyetimuliwa.

Kabla ya Omog, Simba ilikuwa ikinolewa na Mganda, Jackson Mayanja ambaye baadae alikuja kuwa msaidizi wa Omog kabla ya kutemwa.
Makocha wengine ni Dylan Kerr, Goran Kopunovic, Patrick Phiri, Zdravko Logalusic, Abdallah Kibaden na Patrick Liewig.
Kocha Aussems aliyekuwa akilipwa mshahara wa dola 7,000 kwa mwezi wakati akifundisha timu ya taifa ya Nepal  miaka miwili iliyopita.
Mbelgiji huyo aliamua kuacha kazi kwa madai ya wachezaji wa Nepal na viongozi wameshindwa kuonyesha weledi.
Aussems aliandika katika akaunti yake ya Twitter kuwa ameamua kuacha kazi ANFA kwa sababu shirikisho hilo hali kuonyesha kujali kuhusu mipango yake ya kuendeleza soka la Nepali.

No comments

Powered by Blogger.