Full-Width Version (true/false)


Simba: “Yanga wanatuigizia”Wakati ikielezwa kuwa beki ambaye bado hajasaini mkataba mpya na klabu ya Yanga, Kelvin Yondani kutajwa kuelekea upande wa pili, uongozi wa Simba umekana kuhusika na mipango hiyo.

Akizungumza na www.eatv.tv  Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema hakuna ukweli wowote kuhusiana na taarifa hizo huku akidai kuwa ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe.


Manara amesema Yanga wameamua kuvujisha taarifa hizo wenyewe akisema wanajichanga kusaka pesa ili baadaye wakishamsajili waje kusema wameipiga bao Simba.


"Ni muvi ambayo Yanga wanaitengeneza wenyewe, wameamua kuvujisha taarifa hizo makusudi wasake pesa kisha wakija kumsajili waseme wameipiga bao Simba. Sisi hatumuhitaji wala hatuna mpango naye”, amesema Manara.


Manara amesema kuwa hawamuhitaji Yondani wala hawana mpango naye tofauti na taarifa zilivyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumalizana naye.

No comments

Powered by Blogger.