Full-Width Version (true/false)


Singida wasema vita yao dhidi ya Yanga si Kaseke, bali ni hili hapa


Baada ya kukamilisha usajili wa aliyekuwa kiungo wake, Deus Kaseke, uongozi wa Singida United umeeleza kutokuwa na shida yoyote na Yanga juu ya kumsajili mchezaji huyo.

Mkurungenzi wa klabu hiyo kutoka Singida, Festo Sanga, amesema tatizo ambalo wanalo baina yao na Yanga kwa sasa ni kuhusiana na usajili waliofanya kwa Fei Toto.

Sanga ameeleza kuwa kuna mkanganyiko mkubwa kuhusiana na usajili wa mchezaji huyo ambaye amesema walikuwa wameshamalizana kila kitu mbele ya Mwanasheria.

Lakini kati hali ya kushangaza Toto ameibukia Yanga na kutambulishwa mbele ya Waandishi wa Habari pamoja na aliyekuwa mchezaji wa Majimaji, Jaffary Mohammed.

Sanga amefunguka kuwa watakula sahani moja na Yanga dhidi ya Toto huku akieleza hatima yake itamalizwa na bodi ya ligi pamoja na TFF.

No comments

Powered by Blogger.