Full-Width Version (true/false)


Tarimba aamua kuubeba mzigo wa Yondani, Kessy, wakutana na Sanga


Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Abbas Tarimba ameamua kulichukua suala la kuhakikisha Kelvin Yondani na Hassan Kessy wanacheza tena Yanga msimu ujao.Taarifa kutoka kwa mmoja wa Wanayanga kwenye kundi maarufu la klabu hiyo amesema Tarimba atafanya kazi ya kuhakikisha anamalizana na Yondani na Kessy ambao wamebaki Dar es Salaam wakati kikosi hicho kikipaa Nairobi kuifuata Gor Mahia.“Tarimba ameona alichukue hilo suala, unajua ana uzoefu sana na haya masuala ya usajili. Sasa atahakikisha wanabaki,” kilieleza chanzo.Jana, inaelezwa Tarimba alikutana na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga na kuzungumza mambo kadhaa.Awali, ililiezwa wawili hao walikuwa na tofauti na siku chache baadaye Tarimba akaamua kujiondoa katika kamati maalum.Lakini kukutana kwao jana, kumeamsha matumaini mengi makubwa upande wa Wanachama wa Yanga.

Aidha, kumekuwa na taarifa za kwamba Yondani amejiunga na Simba ingawa viongozi wa Simba wamekuwa wakisisitiza suala hilo si kweli.

No comments

Powered by Blogger.