Full-Width Version (true/false)


Timu ya Msuva yaburuza mkia klabu bingwa Afrika

 
Klabu ya Difaa El Jadidi ya nchini Morocco ambayo winga wa kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva anaichezea, imemaliza vibaya katika mzunguko wa kwanza wa hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika. Difaa El Jadidi imemaliza mzunguko wa kwanza wa kundi B bila ya ushindi wowote baada ya usiku wa jumanne kuchapwa 2-1 na wenyeji, ES Setif ya nchini Algeria ambapo katika mchezo huo, Simon Msuva aliingia akitokea benchi.

Simon Msuva aliingia dakika ya 64 kuchukua nafasi ya Chouaib Al Maftoul na kufanikiwa kuamsha hali ya mchezo huo kwa uwezo wake wa kukimbia na mpira.

Mchezo ulidumu kwa sare ya 1-1 kwa kipindi kirefu kabla ya wenyeji kupata bao la ushindi katika dakika za majeruhi za mchezo ambapo kwa kipigo hicho sasa Difaa El Jadidi inakamata nafasi ya mwisho ya kundi hilo ikiwa na alama moja huku TP Mazembe ikiongoza kundi kwa alama 9.

Katika matokeo mengine ya michezo iliyochezwa jana, TP Mazembe imeifunga MC Alger 1-0, Al Ahly ikiichapa Township Rollers 3-0, Zesco United ikitoka sare ya 1-1  na 1 de Agosto huku KCCA ya Uganda ikichapwa 3-2 na ES Tunis .

Matokeo mengine ni, Mbabane Swallows ya Swaziland ikichapwa nyumbani 3-0 na Etoile du Sahel ya Tunisia, Horoya ya Guinea ikitoka sare ya 1-1 na Wydad Casablanca huku Togo Port ikiifunga 1-0 Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini.

No comments

Powered by Blogger.