Trump ajichanganya na kauli yake kuhusu Urusi
Rais
wa Marekani Donald Trump amesema anakubaliana na hitimisho lililotolewa
na Taasisi za Ujasusi za nchi yake kwamba Urusi iliingilia kati
uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwaka 2016.
Akikanusha kauli yake aliyoitoa siku moja iliyopita baada ya mkutano wake na Rais Vladmir Putin wa Urusi.
Amesema
alieleweka vibaya siku ya Jumatatu na kwamba alikuwa akimaanisha kwamba
hakuona sababu kwanini isiwe Urusi ambayo ilifanya udukuzi katika
uchaguzi huo.
Ni
Rais Trump akiitolea ufafanuzi na kuikanusha kauli yake ya awali,
ambayo imezua sintofahamu na kukosolewa vikali. Hata kwa baadhi ya
washirika wake wakitaka ufafanuzi zaidi na kusafisha kauli hiyo.
Amedai
kuwa katika mkutano huo wa Helsinki alimaanisha kusema kwamba hakuna
sababu ya kufikiria kuwa Moscow haiwezi kuingilia kati uchaguzi wa
Marekani.
Amesema ana imani na kuunga mkono taasisi za usalama za nchi yake.
''..Naanza
kusema kwamba nina imani na kuunga mkono mashirika ya kijasusi ya
Marekani na siku zote ni hivyo. Acha niweke wazi kabisa kwa kusema kuwa
na nimekuwa nikisema hivyo mara kadhaa, nakubaliana na hitimisho
lililotolewa wapelelezi wetu kwamba Urusi ilifanya udukuzi katika
uchaguzi uliofanyika mwaka 2016..'' Ameongezea Trump
Lakini
hata hivyo baadhi ya wapinzani wake, wamesema hawana imani na utetezi
huo alioutoa Rais Trump, Huku baadhi yao wakiionya Urusi kwamba
kilichotokea mwaka 2016, kisitokee tena.
Hata
hivyo Kwa upande wake Mark Warner, Seneta kutoka chama cha upinzani
nchini Marekani cha Democratic ameweka wazi kwamba hana imani na kauli
za kiongozi huyo.
''...Sikubaliani
na kauli alizotoa Rais leo. Kama angetaka kutoa kauli hizo, angepaswa
kuwa na uwezo wa kufanya hivyo mbele ya Vladmir Putin. Huyu ni Rais
ambaye alionesha udhaifu mbele ya kiongozi wa Urusi, alionesha udhaifu
mbele ya dunia nzima...'' Alisema Seneta Warner
Credit: BBC
No comments