Full-Width Version (true/false)


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yateua madiwani wanane viti maalum

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteua madiwani wanane wa Viti maalum wa CCM na Chadema kujaza nafasi zilizoachwa wazi.


Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Julai 21, 2018 na mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage inaeleza kuwa uteuzi huo umefanyika katika kikao cha tume hiyo cha Julai 19, 2018.


Walioteuliwa ni Rajabu Kalinga (CCM-Songea), Mary Mbilinyi (CCM-Makete), Zainab Mabrouk (CCM-Kongwa).


Restuta Gardian (CCM-Muleba), Siglinda Ngwega (CCM-Morogoro), Zena Luzwilo (CCM-mji Kahama), Neema Massawe (Chadema-Monduli) na Teodola Kalungwana (Chadema-Iringa).


“Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa waziri mwenye dhamana ya Serikali za mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,” imesema taarifa hiyo.


Imesema nafasi hizo za madiwani ni za Chadema na CCM, baada ya walioteuliwa awali kufariki dunia na kujiuzulu.

No comments

Powered by Blogger.