Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yaahirisha Uchaguzi Kata 4
Tume
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi kwenye kata mbili mpya
na kuahirisha uchaguzi wa kata nyingine nne. Mabadiliko hayo yanafanya
jumla ya kata zenye uchaguzi kuwa 77 badala ya 79 zilizotangazwa awali.
Akizungumza
jana Julai 10, Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa NEC, Jaji
Semistocles Kaijage amezitaja kata hizo mpya kuwa ni Kelamfua ya
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Kata ya Kitaya, Halmashauri ya Wilaya
ya Nanyamba.
“Kwa
mujibu wa Kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa aliitaarifu Tume uwepo
wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata ya Kelamfua iliyoko katika
Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Kata ya Kitaya iliyoko katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba,” alisema Jaji Kaijage.
Jaji Kaijage alisema kwamba nafasi zote mbili za Udiwani zimetokana na kujiuzulu kwa madiwani waliokuwa wamechaguliwa awali.
Alisema
uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Julai 16 na kampeni zitaanza
Julai 17 mpaka 11 Agosti na siku ya kupiga kura ni Agosti 12.
Jaji Kaijage amevialika vyama vya siasa, wadau wote wa uchaguzi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi huo.
Katika
hatua nyingine Jaji Kaijage ametangaza kuahirishwa kwa uteuzi wa
wagombea kwenye kata tatu za Tindabuligi, Kisesa, Katumba na Mlimba.
Tume itatangaza hapo baadae tarehe nyingine za uteuzi na uchaguzi katika kata hizo.
No comments