Full-Width Version (true/false)


Tunduru wakulima watahadharishwa kutapeliwa Pembejeo.Wakulima wa zao la Korosho katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma wametaadharishwa kuwa makini na matapeli wanaouza pembejeo feki zilizochanganywa na unga wa muhogo na badala yake wametakiwa kununua pembejeo zinazosambazwa na bodi ya korosho tawi la Tunduru. 

Kauli hiyo iemtolewa na mkuu wa wilaya ya Tunduru Bw.Juma Homela katika mikutano yahadhara na wakulima wa zao la Korosho kuelezea upatikanaji salama wa pembejeo katika kipindi hiki cha upuliziaji wa mikorosho.  

Kwa upande wake neneja wa bodi ya Korosho tawi la Tunduru Mokiwa Shauri anasema bodi hiyo inapembejeo za kutosha, huku wakulima wakiomba pembejeo kuwakia kwa wakati ili kuondokana na suala la kutapeliwa.

No comments

Powered by Blogger.