Full-Width Version (true/false)


UN yaitaka Tanzania kupambana dhidi ya ukeketaji
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani UNFP limesema  jitihada za haraka zinahitajika nchini Tanzania kupambana na aina mpya ya ukeketaji wa watoto wadogo walio chini ya mwaka mmoja jambo linaloathiri na kurudisha nyuma maendeleo ya mtoto wa kike.

Mwakilishi na Mshauri wa Shirika hilo nchin Anna Holmstrom amezungumza hayo katika uzinduzi  wa filamu ya kitanzania  ya “in the name of your daughter” inayoelezea maisha ya changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike kutokana  ukeketaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha wanawake  wanahabari nchini Tanzania TAMWA Eda Sanga amesema kuwa bado elimu inahitajika pamoja na  ili kupunguza janga ili ambalo linakiuka haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya malaria Tanzania 2015-16 uliotolewa na NBS ilibainisha kuwa bado kuna baadhi ya mikoa nchini ikiwemo manyara ambayo zaidi ya nusu ya wanawake  wamekeketwa.

No comments

Powered by Blogger.