Full-Width Version (true/false)


Ustaa wa Salamba wateka mazoezi Simba


KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki wa Simba juzi walim­vamia kaimu kocha mkuu wa timu hiyo Mrundi, Masoud Djuma na kuanza kulalamikia aina ya uchezaji wa msham­buliaji wake mpya, Adam Salamba.
 
Tukio hilo la aina yake lilitokea juzi Jumatatu jio­ni mara baada ya mazoezi ya timu hiyo kumalizika Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.
 
Salamba, alisaini mkataba wa kuichezea timu hiyo hivi karibuni kwa dau la shilingi milioni 40, huku akipewa gari na nyumba ya kuishi aki­tokea Lipuli FC ya mkoani Iringa.
 
Kundi hilo la mashabiki walim­vaa kocha huyo na kumwam­bia anatakiwa kukaa kikao na msham­buliaji huyo na kumwam­bia aache kucheza kistaa kwani bado ana sa­fari ndefu katika soka.
 
“Tunakuomba kocha ukae na Salamba na ku­muonya kuwa yeye bado hajakuwa staa ndani ya Simba, ndiyo kwanza amesajiliwa hivi kar­ibuni hana hata msimu mmoja.
 
“Katika michuano hii Kagame tumekuwa tukimfuatilia uwanjani akicheza kistaa kama ameshakuwa levo za akina Ronaldo (Cristiano) na Messi (Lionel) kitu ambacho siyo sawa, anatakiwa kubadilika na afahamu yeye bado.
 
“Kwa sababu ukimuacha aendelee kucheza kistaa mwisho wa siku ataigharimu timu kwa kupata matokeo mabaya, anatakiwa kucheza kwa kupambana kama alivyokuwa Rashid (Mohamed) na Marcel (Boniventure),” alisikika shabiki wa Simba huku kocha huyo akiitikia.
 
Kocha huyo al­imjibu shabiki huyo kwa kumwambia: “Hicho unach­okizungumza ni kweli kabisa, mimi nimeliona hilo na kulifanyia kazi na nilikaa naye kikao na kumuonya anatakiwa kubadi­lika na kunia­hidi.

No comments

Powered by Blogger.