Full-Width Version (true/false)


Utendaji wa Rais Magufuli wavunja ngome ya CUF


UTENDAJI wa Rais John Magufuli na Mbunge wa Rufiji, Mohamed Mchengerwa,umevunja ngome ya chama cha wananchi (CUF) kwa kuwang’oa viongozi pamoja na  wanachama wake zaidi ya 180.


Viongozi na wanachama hao walitangaza kukihama chama hicho na kutimkia Chama Cha Mapinduzi (CCM) juzi katika ziara ya Mchengerwa iliyofanyika kijiji cha kipoka kata ya Chumbi.


Katika mkutano huo viongozi waliotimkia CCM ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF kata ya Chumvi,Khamis Kivurugwe na  Katibu wa chama hicho Juma Mnondo .


Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachama hao wapya wa CCM walisema wamefurahishwa na utendaji kazi wa Dk Magufuli ambao umewajali watu wa Rufiji kwa kuruhusu ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha MW 2100 kwa kutumia maporomoko ya maji katika mto Rufiji (Stiegler’s Gorge ) unaojengwa katika kata ya Mwaseni ambao utawanufaisha na kusahau shida ya umeme.


“Tulifurahi sana baada ya kusikia kuwa serikali inatupatia umeme Rufiji nzima na wakati wa ujenzi wa umeme huo vijana na kina mama watapata kazi za kufanya,kwa utaratibu huu kwanini tubaki upinzani? Tunataka maendeleo sio porojo za viongozi wetu,Dk Magufuli ametumaliza”alisema Kivurugwe


“Mimi nilikuwa mgumu sana kipindi cha uchaguzi mkuu nilimpinga Magufuli  na Mchengerwa lakini sasa nimesalimu amri na timu yangu yote inarudi (CCM),naombeni kadi ili tufanye kazi kwa kushirikiana tuijenge Rufiji tunayoitaka”aliongeza


Kivurugwe  alisema tangu serikali ya awamu ya tano iingie madarakani wananchi wa Rufiji wamenufaika hivyo hawaoni sababu ya kuendelea kubaki vyama upinzani kutokana .


Kwa upande wake Mnondo alisema wananchi hao wamenufaika pia na maji kwa kuchimbiwa visima,kujengewa zahanati katikia maeneo tofauti  jambo ambalo halijawahi kutokea katika historia yao hivyo hawana budi kuunga mkono juhudi za viongozi hao za kuujenga mji wao.


“Pamoja na pongezi hizi mheshimiwa  Mbunge tunaomba utuombee hili daraja lililopo eneo la mwake ambalo lilianza kujengwa likamilike kwani tunashindwa kusafiri kwa kuwa njia haipitiki,kwakuwa mambo mengi tuliyoomba mmetusaidia tuna imani na hili litataftiwa ufumbuzi’’alisema Mnondo


Kwa upande wake Mchengerwa alisema serikali hii imedhamiria kwa dhati kuwasaidia wananchi wanyonge hivyo changamoto zao zitataftiwa ufumbuzi na kwamba serikali imetenga fedha ya kujenga barabara kutoka Nyamwage Utete kwa kiwango cha lami.


“Pongezi zenu kwetu na kwa serikali zinazidi kutupa nguvu ya kuwatumikia niwaahidi tutapiga kazi nzuri sana,hamtajuta kurudi CCM,hamjakosea kwani Dk Magufuli anatekeleza kwa vitendo ilami ya CCM “alisema Mchengerwa

No comments

Powered by Blogger.