Full-Width Version (true/false)


Vigogo Kesi ya Uhujumu Uchumi wa Madini ya Almasi Kuendelea Kusota Mahabusu

Jalada la kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mkurugenzi wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort),  Archard Kalugendo na mthamini almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kwa ajili ya uamuzi.

Wakili wa Serikali, Mutalemwa Kishenyi amedai hayo jana Jumatatu, Julai 16, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo inayowakabili waajiriwa hao wa Wizara ya Madini, ilipotajwa.

Kishenyi alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika akibainisha kuwa jalada la shauri hilo lipo kwa DPP kwa ajili ya kulipitia na kulifanyia uamuzi.

Baada ya kueleza hayo aliomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Julai 30, 2018.

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na DPP kuzuia dhamana zao.

No comments

Powered by Blogger.