“Vyakula vya harusini vichunguzwe”-Waziri Ummy

Waziri
Ummy Mwalimu ametoa maagizo hayo, alipotembelea kuangalia ujenzi wa
jengo la TFDA ambalo linajengwa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa
wananchi wa mkoa huo.
Waziri
Ummy amesema kuwa vyakula hivyo vimekuwa vikisafirishwa umbali mrefu
bila kujua vinaandaliwa katika mazingira yapi na kubebwa kwa usalama wa
hali gani ili kulinda afya za walaji.
“Hatutaki
kuharibu biashara za wajasiriamali wa vyakula lakini tunahitaji
kufahamu mazingira ya uandaaji wa vyakula hivyo pamoja na vifungashio
wanavyotumia, kuna familia imewahi kulazwa Muhimbili mara baada ya kula
chakula harusini na hivyo nawapa agizo hilo mkalifanyie kazi”, amesema Waziri Ummy.
Mbali
na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania
isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo wanatakiwa
kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
No comments