Full-Width Version (true/false)


Wachezaji wa Barcelona, Atletico na Real Madrid waweka rekodi ya kipekee kwenye fainali ya kombe la duniaYakiwa yamebakia masaa kadhaa kuanza  kwa mchezo wa  fainali ya Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi  , tayari  klabu kubwa  tatu kutoka  Hispania   wachezaji   wao   watashinda kombe hilo kwa namna yoyote ile.

Klabu ya Barcelona ,  Real  Madrid na  Atletico  Madrid  ndio  klabu  zilizotoa wachezaji  wengi     kwenye   mchezo  wa fainali  kati ya   Croatia na   Ufaransa, wachezaji  watatu kwa kila timu.
Wachezaji wa Barcelona watakaotumikia leo timu zao za taifa ni Samuel Umtiti , Ousmane Dembele  wote Ufaransa na  Ivan Rakitic wa Croatia.
Samuel Umtiti , Ousmane Dembele
Wachezaji kutoka Real Madrid ni Luka Modric na   Mateo Kovačić   wote wa Croatia   huku Raphael Varane  akiitumikia Ufaransa.
Luka Modric na   Mateo Kovačić
Kwa upande wa Atletico Madrid , wachezaji watakaoiwakilisha klabu hiyo kwenye mchezo wa fainali ni   Sime Vrsaljko kutoka  Croatia na   Lucas Hernandez  na   Antoine   Griezmann   wote wa Ufaransa.
Lucas Hernandez  na   Antoine   Griezmann
Katika maana nyingine ni kwamba klabu hizo kwa matokeo yoyote yale ni lazima  wachezaji wao wachukue kombe la Dunia leo.

No comments

Powered by Blogger.