Full-Width Version (true/false)


Wachezaji Yanga wagomea mazoezi

 

Yanga hali bado si shwari baada ya wachezaji wake Andrew Vincent ‘Dante’ na Beno Kakolanya kugomea kufanya mazoezi kutokana na mabosi wa timu hiyo kuwapiga chenga katika suala la fedha za usajili.
Awali mabosi wa Yanga akiongozwa na Mwenyekiti wa Usajili, Hussein Nyika alizungumza na wachezaji hao kwaajili ya kuongeza mikataba na wakakubaliana kila kitu na kuwaambia waanze mazoezi kujiandaa na mchezo dhidi ya Gor Mahia.
Pamoja na wachezaji hao kuanza mazoezi wakisubilia fedha zao za usajili mpya, lakini hali imekuwa tofauti baada ya kupigwa danadana hali ambayo imewafanya kuanza kujiondoa polepole.
Mwanaspoti limepenyezewa kuwa Dante na Kakolanya hawajaenda mazoezini baada ya kuona timu yao inasajili huku wao wakipotezewa na kuambiwa wasaini kisha watapewa fedha wakati wachezaji wapya wanalipwa.
Uongozi wa timu hiyo kabla ya kuanza mazungumzo mapya ya mkataba na wachezaji hao, waliwalipa madeni ya nyuma waliyokuwa wanadai, lakini bado wanataka kuwakopa mikataba mipya.

No comments

Powered by Blogger.