Full-Width Version (true/false)


Wakazi wa Mwanza waahidiwa neema na Mbunge wao
Na Paschal D. Lucas, Mwanza
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana na Meya wa zamani wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula amendelea kutekeleza ahadi yake kwa wananchi ikiwemo ya ujenzi wa barabara zote zilizopo katikati ya jiji la Mwanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mabula ameyasema hayo leo Julai 16,2018 kwenye kipindi cha Pambazuko cha kituo cha radio cha Metro Fm kilichopo Mwanza kilichokuwa kinataka kufahamu utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

"Jiji la Mwanza limeongoza kwa usafi mara nyingi sana nikiwa Meya,naamini juhudi hizo naendelea nazo na kwa kuwa jiji la Mwanza linazidi kukua na kupanuka kwa sasa tumesaini mkataba wa ujenzi wa barabara na kampuni ya Nyanza road kujenga barabara zote zilizopo katikati ya jiji la Mwanza kwa kiwango cha lami na sio kuziziba ziba ni kuzifumua zote na kuweka lami". Alisema Mabula.

Kwa upande wa afya amesema kuwa kwa jimbo la Nyamagana kutakuwepo na vituo vya afya vinne vyenye hadhi na vyenye mahitaji yote ya muhimu kwa huduma ya afya ili kutoa na kusaidia utoaji na upatikana kwa urahisi wa huduma za afya.

Aidha amewaomba wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na viongozi kwa kutoa ushirikiano katika kuboresha miundombinu ikiwemo ya barabara,hospitali,vituo vya afya na shule ili kuwezesha upatikanaji wa huduma kwa haraka.

No comments

Powered by Blogger.