Full-Width Version (true/false)


Wakenya wacharuka wabunge kusafiria fedha za umma
Wakenya wamekasirishwa na taarifa kwamba wabunge 20 wamesafiri kwenda Urusi kutazama kombe la dunia kwa gharama ya fedha za umma.


Wamekwenda kutazama mechi nne, ikiwemo fainali kati ya Ufaransa na Croatia, katika safari ya wiki mbili inayokadiriwa kuwa na thamani ya maelfu ya dola.


Mjadala ulizuka baada ya wabunge hao kuweka picha walizopiga uwanjani.


Waziri wa michezo Rashid Echesa ameiambia BBC kwamba alitoa idhini kwa wabunge 6 pekee kusaifiri, kusaidia kuelewa jinsi matukio makubwa ya kimataifa yanavyoandaliwa.


Kenya haijawahi kufuzu kwa fainali ya Kombe la Dunia na imeorodheswha nafasi ya 122 kati ya matifa 206 na shirikisho la soka duniani FIFA.


Hatahivyo Kenya ina umaarufu mkubwa katika riadha na ni mojawapo wa mataifa yenye ufanisi mkubwa duniani .


Tayari nchi hiyo imewasilisha ombi la kutaka kuwa mwenyeji mashindano ya kimataifa ya riadha mwaka 2023.


Lakini hisia iliopo kwa Wakenya ni kwamba safari hiyo ni upotezaji wa fedha za umma katika nchi ambayo kipato cha mtu wa kawaida ni $150 kwa mwezi.


Katika maoni yaliopo huyu anastaajabishwa na hatua hiyo akieleza kwamba huwezi kuwaona viongozi wakitazama hata mechi za ndan ya nchi kuinusha talanata ya ndani lakini wabunge wana muda wa kujigamba kwa picha Urusi.

No comments

Powered by Blogger.