Full-Width Version (true/false)


Wanakijiji wauwa mamba 300 kulipiza kisasi cha kijana waoWanakijiji magharibi mwa Papua nchini Indonesia wamewauwa takribani mamba 300 waliyokuwa wakipatikana kwenye sehemu ya hifadhi baada ya kijana mmoja kushambuliwa hadi kufa.

Picha kadhaa zimeenea kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha wananchi hao wakiwa na silaha za jadi, mapanga, nyundo na visu baada ya kufanya tukio hilo la kulipiza kisasi.

Maafisa na polisi wanasema kuwa hawakuweza kuzuia mauaji hayo lakini watafungua mashtaka dhidi ya waliohusika.

Kwa mujibu wa sheria za nchini Indonesia mtu yeyote anayekutwa na hatia ya kuuwa wanyama wanaopatikana kwenye hifadhi adhabu yake inaweza kuwa ni kifungo jela.

Kijana huyo alishambuliwa na mamba siku ya Ijumaa kisha kuzikwa Jumamosi ndipo wanakijiji hao wakaingia wenye hifadhi hiyo na kuwauwa mamba wote.

No comments

Powered by Blogger.