Full-Width Version (true/false)


Wananchi wawajengea Askari Polisi Nyumba Za Kuishi
WANANCHI wa Kijiji cha RUBANDA Wilayani Serengeti Mkoani Mara wamewajengea nyumba za kuishi Askari Polisi waliopo katika eneo lao.
Hiyo ni kutokana na ushirikiano uliopo kati yao huku wengine wakimuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro kuwaongezea magari ya Polisi katika Wilaya hiyo kutokana na miundombinu yake jambo ambalo litawawezesha kuzuia uhalifu kabla haujatokea.Wananchi hao wameyasema hayo wakati wa Ziara ya IGP Sirro inayoendelea katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, kwa lengo la kubaini changamoto za kiuhalifu na kuzipatia ufumbuzi wa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa Amani na utulivu.
Kwa Upande wake IGP amekubaliana na ombi hilo pamoja na kutoa tathmini fupi ya hali ya usalama hapa nchini ambapo amesema hali inaendelea kuwa shwari.


Katika hatua nyingine  IGP Sirro ametoa ushauri kwa Wakazi wa Kijiji hicho kusomesha watoto wao ili wasiwe tegemezi na kujiingiza katika vitendo vya kihalifu.

"Chonde chonde naomba tuwe na watoto wachache tuweze kuwasomesha watoto wachache ili umsomeshe mtoto kesho achukue nafasi mahali hakuna sababu ya kurundika watoto wengi halafu baadae tunashindwa kuwasomesha wanakuwa na maisha baade sio mazuri inakuwa haipendezi" IGP SIRRO amesema

 IGP anaendelea na ziara yake huku akitumia usafiri wa Helkopta ili kujionea kwa uhalisia maeneo hayo, pia kuweza kuzipatia ufumbuzi changamoto za kihalifu.

No comments

Powered by Blogger.