Full-Width Version (true/false)


Wananchi wenye hasira kali watibua ziara ya Rais Donald Trump nchini Uingereza

 

Rais wa Marekani, Donald Trump jana Julai 12, 2018 alipokelewa kwa maandamano makali nchini Uingereza kwenye ziara ya kikazi ya siku nne nchini humo.


Maelfu ya raia wa Uingereza ambao walipinga ziara hiyo ya Rais Trump mapema mwaka huu, wamejitokeza kwenye maandamano hayo leo tena katika eneo viunga vya bunge la Uingereza na barabara kubwa jijini London wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti.

Hata hivyo bado maandamano hayo hayajazuia chochote kwani Rais Trump leo anatarajiwa kuonana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May na kesho akiwa na mkewe, Melania Trump watamtembelea Malkia Elizabeth.


No comments

Powered by Blogger.