Full-Width Version (true/false)


Watanzania waliokimbia vurugu Msumbiji waruhusiwa


 

Watanzania 544 waliokuwa wakiishi kwenye kambi ya muda katika kijiji cha Chivava wilaya ya Mtwara wameruhusiwa kuondoka ili kuendelea na shughuli nyingine.
 Watanzania hao walikuwa wakiishi Msumbiji katika kijiji cha Kisungule na waliingia nchini Julai 11 wakikimbia vurugu nchini humo.
Kadhalika, raia 92 wa Msumbiji waliokuwa wakiishi kwenye kambi hiyo, wataendelea kuhifadhiwa hadi taratibu nyingine zitakapochukuliwa.
Akizungumza leo Julai 13 baada ya kutembelea kambi hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa alisema raia hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao baada ya serikali kujiridhisha hali ni shwari.
Wakazi hao walikimbia vurugu zilizotokea kijiji cha baada ya kikundi cha watu wasiofahamika kuanza kufanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuvamia kituo cha polisi.
“Tulitaka tujiridhishe kwanza tunaowapokea wako salama kiasi gani, hatuna sababu nyingine tena tuendelee kuwashikilia watanzania ambao mna makazi yenu na maeneo ambayo mnaweza kuishi,”amesema Byakanwa
Awali akisoma taarifa ya kambi, Luteni Kanali, Elvice Massawe amesema  miongoni mwa waliopokelewa na kuwekwa kambini 27 waligundulika kuwa na ugonjwa wa malaria,106 walikuwa na magonjwa mchanganyiko  huku mmoja amepewa rufaa kwenda hospitali ya Rufaa ya Ligula  baada ya kubainika kuwa na upungufu wa damu.No comments

Powered by Blogger.